Search This Blog

Saturday, July 3, 2021

Mbunge Paulina Gekul afanya ziara soko kuu la Babati.


Na John Walter-Babati

Mbunge wa Jimbo la Babati mjini  ambae pia ni Naibu Waziri wa Habari,utamaduni Sanaa na Michezo Paulina Gekul, amefanya ziara kwa kutembelea na kusikiliza wafanya biashara wa soko kuu la Babati na kusikiliza  kero na changamoto zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi.

Akizungumza na wafanyabiashara hao Mheshimiwa Gekul mbali na kuelezea juu ya mikakati na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha wafanya biashara hao wanakuwa na mazingira mazuri na bora ya kibiashara sokoni hapo, amewahakikishia ushirikiano kama Mbunge wa Jimbo lao.

Akimkaribisha mbunge, Mwenyekiti wa soko mbali na kuwataka wafanya biashara kuwa wawazi kwa kuelezea changamoto zinazowakabili amemshukuru Gekul kwa uamuzi wake wa kuamua kulitembelea soko na kuzungumza na wafanyabiashara hao.

Aidha akiwa ameaambatana na Mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange na mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Babati walikitembelea choo kinachotumika sokoni hapo na kujionea vilivyojaa kwa kukosa chemba inayowezesha kubeba maji taka.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange ameagiza choo hicho kifanyiwe marekebisho kuanzia jumatatu huku majitaka yaliyojaa katika chemba hiyo yakianza kutolewa kuanzia sasa.

Kwa upande mwingine mkuu huyo wa wilaya ametoa muda wa wiki moja kwa halmashauri ya mji wa Babati kuhakikisha taa zinafungwa katika soko hilo kuwawezesha wafanyabiashara kufanya biashara zao hata wakati wa usiku.

Gekul anafanya ziara katika kata nane za jimbo hilo akizungumza na makundi mbalimbali na kufanya mikutano ya hadhara kuwashukuru kwa kumuamini,  na kusikiliza kero zinazowakabili akiwa ameambatana na wataalamu wa idara mbalimbali ili kujibu maswali ya wananchi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...