Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa, amekemea tabia ya baadhi ya viongozi wa serikali kujikweza na kunyanyua mabega kiutawala na kuacha kuwasaidia wananchi ambao ndo waajiri wao katika huduma mbalimbali.
Kauli hiyo ameitoa Jiji Dodoma ambapo amebainisha kuwa matatizo makubwa yanayotokea katika maeneo ya kazi kwa baadhi ya viongozi kujikweza kiutawala na wizi wa mali za umma umesabishwa na baadhi ya watumishi kukosa weledi wa uendeshaji wa taasisi za umma.
Kufuatia kauli hiyo Mchengerwa akawataka watumishi wa umma kuacha kujiona wanahaki zaidi kuliko watu wengine kwakuwa kila eneo wameweka watu wakufuatilia namna shughuli za serikali zinavyoendeshwa ili ziendane na mahitaji ya wananchi.
Katika hatua nyingine Mhe. Mchengerwa amesema kwa sasa wanafanya uchambuzi na mapitio ya watumishi 18,000 ambao ni sehemu ya madai ambao wataigharimu serikali shilingi bilioni 11 fedha ambazo tayari Rais wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, ameshazikabidhi ofisi ya utumishi kwa taratibu zaidi kufanyika.

No comments:
Post a Comment