Search This Blog

Tuesday, July 27, 2021

Marekani kusaidia operesheni za anga Afghanistan

Marekani ilitangaza kuwa itaendeleza msaada wake wa anga kwa vikosi vya Afghanistan katika wiki zijazo dhidi ya Taliban, ambayo imeongeza mashambulizi yake.

Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Kati cha Marekani (CENTCOM) Kenneth McKenzie aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba walitoa msaada wa anga kwa mapambano yanayoendelea ya vikosi vya Afghanistan dhidi ya Taliban karibu na Kandahar.

McKenzie alisema,

"Marekani imeongeza operesheni zake za anga kwa msaada wa vikosi vya Afghanistan katika siku chache zilizopita. Tumejiandaa kuendelea na msaada huu katika wiki zijazo ikiwa Taliban wataendelea na mashambuliz yao."

McKenzie alisisitiza kuwa wataendelea kutoa msaada wa vifaa kwa vikosi vya Afghanistan hata baada ya uondoshaji wa wanajeshi kutoka nchi hiyo kukamilika mnamo Agosti 31.

Kuhusiana na kuongezeka kwa mashambulizi ya Taliban, McKenzie alieleza kuwa serikali ya Afghanistan inakabiliwa na wakati mgumu, lakini itakuwa wazi ndani ya siku na wiki kadhaa kwamba serikali inaweza kuitetea nchi hiyo dhidi ya Taliban.

Katika taarifa ya hivi karibuni kutoka CENTCOM, iliripotiwa kuwa takriban asilimia 95 ya majeshi ya Marekani kujiondoa Afghanistan imekamilika.

Wakati mchakato wa amani nchini Afghanistan bado haujabainika, mapigano makali kati ya vikosi vya usalama na Taliban yanaendelea.

Kulingana na taarifa za shirika la habari la Anadolu Agency (AA) kutoka kwa serikali za mitaa, Taliban wamekamata wilaya zaidi ya 150 kati ya 407. Taliban, kwa upande mwingine, inashikilia msimamo kwamba idadi ya vituo vya wilaya chini ya udhibiti wao ni 256.

Nchini humo, mikoa 34 iko chini ya udhibiti wa vikosi vya serikali kuu.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...