Search This Blog

Thursday, July 8, 2021

Kiongozi wa wanamgambo DRC akamatwa


Polisi katika Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo wamemkamata kiongozi wa wanamgambo wa Mai Mai, Kambale Kabamba.

Alikamatwa katika eneo la Kyona, katika wilaya ya Pakanza katika mji wa Oicha (Beni territory), Kivu Kaskazini.

Polisi wamekuwa wakimsaka juu ya kuhusika kwa mashambulio katika eneo hilo.

Atafikishwa katika mahakama ya kijeshi kuwajibishwa kwa vitendo vyake.

Kuna makundi kadhaa ya wanamgambo katika jimbo la DRC la Kivu Kaskazini.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...