Search This Blog

Thursday, July 8, 2021

Botswana yafichua almasi kubwa ya mwezi


Jiwe hili la Almasi limeripotiwa kuwa ni la tatu kwa ukubwa dunianiImage caption: Jiwe hili la Almasi limeripotiwa kuwa ni la tatu kwa ukubwa duniani

Botswana imefichua jiwekubwa na jeupe la almasi lenye ukubwa wa karati 1,174, liliwa ndio jiwe la pili kwa ukubwa kuchimbuliwa nchini humo mwezi huu.

Almasi hiyo iligunduliwa tarehe 12 Juni na kampuni ya machimbo ya madini ya Canada- Lucara na kuwasilishwa kwenye hifadhi ya taifa ya madini iliyopo katika mji mkuu Gaborone Jumatano.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo Naseem Lahri ameliambia shirika la habari la AFP kwamba Almasi hiyo ni ya tatu kwa ukubwa duniani.

"Hii ni historia kwetu na kwa Botswana pia ," alisema.

Mwezi uliopita, jiwe lililokuwa na uzito wa karati 1,098 -lilionyeshwa kwa Rais Mokgweetsi Masisi, baada ya kampuni ya almasi ya Debswana, kuligundua tarehe 1 Juni.

Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi aliushirikisha umma picha za jiwe hilo la thamani :



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...