Timu ya taifa ya England imeinga hatua ya fainali ya Euro 2020 baada ya ushindi wa mabao 2-1 mbele ya timu ya taifa ya Denmark kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali baada ya kushindwa miaka 55 bila kutinga katika hatua hiyo mara ya mwisho ikiwa ni mwaka 1966.
Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Wembley ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo vijana wa Kocha Mkuu, Gareth Southagate ilibaki kidogo wafike hatua ya penalti kutokana na kufika katika dakika za nyongeza.
Sasa watakutana na Italia ambao walishinda kwa penalti 4-2 mbele ya Hispania baada ya kufungana bao 1-1. Mchezo huo wa fainali ambao utaamua nani atakuwa bingwa wa Euro 2020 unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Wembeley, Jumapili.
No comments:
Post a Comment