John Walter-Babati.
Mkazi wa kijiji cha Mutuka wilayani Babati Mkoa wa Manyara, Emmanuel Naasi (30) anasakwa na polisi akituhumiwa kumbaka na kumuua mtoto wa kaka yake mwenye umri wa miaka mitano.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Marrison Mwakyoma amesema tukio hilo limetokea Julai 5, 2021 saa 12 jioni na kwamba Naasi alikutana na mtoto huyo na wenzake wawili wakitoka kuchota maji na kuanza kuwakimbiza
Amesema watoto wawili waliokuwa na marehemu ndio waliokwenda kutoa taarifa kijijini na shughuli ya kutafuta mwili ikaanza na kupatikana saa 2 usiku.

No comments:
Post a Comment