Search This Blog

Wednesday, July 7, 2021

Hali ya tahadhari yatangazwa New York kufuatia ghasia za bunduki


Polisi wanawake wanaohusika na masuala ya kijamii wakiwa kaziniImage caption: Polisi wanawake wanaohusika na masuala ya kijamii wakiwa kazini

New York Governor Andrew Cuomo ametangaza hali ya tahadhari kufuatia kuongezeka ghafla kwa visa vya ufyatuaji risasi katika jimbo hilo.

Gavana alisema kuwa zaidi ya watu 51 wameuawa baina ya wikendi ya Julai 4.

Kumekuwa na ongezeko kubwa la vifo vitokanavyo na mashambulio ya bunduki kote nchini Marekani, ambapo vifo 200 vilitokea mwishoni mwa juma pekee katika maeneo mbali mbali ya Marekani.

Agizo hilo litakwenda sambamba na kutengwa kwa dola milioni 138.7 kwa ajili ya mipango ya kuingilia kati na kuzuia ghasia za bunduki.

Kuanzia mwezi Mechi hadi Mei mwaka jana, 2020, kulikuwa na ongezeko la mashambulizi na uhalifu wa kutumia bunduki katika jimbo la New York State na katika maeneo mengi ya Marekani.

Gavana aliamua kuchukua uamuzi wa kuongeza usalama katika maeneo yenye hatari ya kiusalama, pamoja na kutoa mafunzo ya kazi kwa watu wanaoishi katika maeneo masikini.

IMwezi Machi, shirika la ujasusi la Marekani FBI lilitoa ripoti ya awali ya takwimu za mwaka 2020 zilizoonesha kupanda kwa asilimia 25 kwa mauaji -ikilinganishwa na mwaka uliopita . ongezeko hilo limeendelea kupanda katika mwaka 2021.

nchini Marekani vifo vingi vya nyumbani huthusishwa na bunduki .



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...