Search This Blog

Thursday, July 15, 2021

Azam FC: Lazima tuipe Simba heshima yake


Kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Simba, uongozi wa Azam FC umesema utaipa timu hiyo heshima yake kama mabingwa 'guard of honour' kwa sababu ndiyo taratibu na uungwana katika soka.

Azam inatarajia kuikaribisha Simba kesho katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu ya Azam, Thabit Zakaria 'Zaka Zakazi' amesema watawapigia makofi ya heshima Simba ili kuendeleza utamaduni wa soka unaofanyika duniani.

"Hii si mara ya kwanza kufanyika hapa Tanzania, mara ya kwanza kabisa Tanzania tulifanyiwa sisi Azam tulivyokuwa mabingwa msimu wa 2013/2014 tulivyocheza na JKT Ruvu.

Kwa sababu sisi tulifanyiwa kwa mara ya kwanza, tutarudisha hiyo heshima, hili ni jambo zuri kwa kuwa mpira tunaocheza una utamaduni na taratibu zake," amesema Zaka Zakazi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...