Search This Blog

Saturday, June 12, 2021

Spika wa zamani wa Iran adai maelezo ya kunyimwa kushiriki uchaguzi Mkuu


Spika wa zamani wa Bunge la Iran Ali Larijani ametaka kupewa maelezo kutoka kwa tume ya uchaguzi juu ya sababu ya kunyimwa nafasi ya kushiriki katika uchaguzi Mkuu wiki ijayo. 

Mwezi uliopita tume hiyo iliwaidhinisha wagombea saba pekee kushiriki uchaguzi huo wa siku ya Ijumaa na kuwanyima nafasi hiyo wagombea mashuhuri akiwemo Larijani na aliyekuwa rais wa Jamhuri hiyo ya kiislamu Mahmoud Ahmadinejad. 

Hatua hiyo ya kuwanyima fursa ya kushiriki wagombea mashuhuri nchini humo itaongeza uwezekano wa kuibuka mshindi Jaji Mkuu wa Iran Ebrahim Raisi, ambaye ni mshirika wa kiongozi wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...