Search This Blog

Thursday, June 17, 2021

RC Songwe azitaka Halmashauri kutoa elimu kwa wazazi uchangiaji chakula cha mchana shuleni


Na, Baraka Messa, Songwe

MKUU wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba ameziagiza Halmashauri zote za mkoa wa Songwe kutoa elimu kwa wazazi kuhusu umuhimu wa chakula Cha mchana katika shule zote kuanzia awali mpaka Sekondari ili kuimalisha elimu na kuongeza kiwango cha ufaulu .

Mkuu wa mkoa amesema hayo  Jana  kwenye kikao Cha wadau wa elimu Mkoa wa Songwe kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Vwawa wilayan Mbozi.

Alisema changamoto ya chakula cha mchana katika shule za Awali, Msingi na Sekondari ni kubwa kutokana na wazazi kutoshirikishwa vizuri na kufahamishwa kwa kupewa elimu kuhusu umuhimu wake katika maendeleo ya watoto wao.

Alisema kuna umuhimu mkubwa wa wazazi wa watoto wanaosoma pamoja na jamii kwa ujumla kushirikishwa kwa kupewa elimu namna ya kushiriki katika kuchangia chakula Cha watoto ambao wengi wanatembembea umbali mrefu kufwata masomo .

"Ni muhimu wazazi kupewa elimu kuhusu uchangiaji wa chakula Cha lishe shuleni  ili kuimalisha afya za watoto na kuelimisha ufaulu , kwenye kipengele Cha  wazazi kushirikishwa bado hatujafanya vizuri wazazi bado hawajapewa elimu ya kutosha Halmashauri zote tukatoe elimu kwa wazazi , viongozi wa mitaa, vijiji na Kata zote mpaka Wilaya na Mkoa" alisema Mkuu wa Mkoa.

 Alisema wananchi kwa kuwa hawajashirikishwa vizuri bado wanaamini kuwa shughuli za chakula, ujenzi wa miundo mbinu katika shule zinazowazunguka hasa madarasa, vyoo na  madawati kuwa ni jukumu la Serikali pekee Jambo ambalo sio sahihi.

"Kiuhalisia wananchi wanatakiwa kushiriki kwenye shughuli za ukamilishaji miundo mbinu ya shule ili kuboresha mazingira ya ujifunzaji , wananchi wasipojitoa kwenye uchangiaji wanawaweka katika mazingira magumu watoto wao ambao wanahitaji mazingira rafiki" alisema Mgumba

Afisa Elimu Mkoa wa Songwe Juma Kaponda alisema pamoja kiwango cha ufaulu kuongezeka bado kunachangamoto ya wazazi kuchangia chakula Cha mchana kwa watoto kutokana na wazazi wengi kutojua umhimu licha ya kuambiwa mara nyingi.

Alisema Mkoa umefikia asilimia 50 ya utoaji chakula kwa shule zote za Msingi na Sekondari, huku akieleza kuwa shule hizo zinazotoa chakula sio watoto wote wanapata chakula Cha mchana kutokana na baadhi ya wazazi kutochangia kabisa.

"Kwa kawaida mtoto mdogo inatakiwa ale angalau Milo mitatu ili kuimalisha afya na ujifunzaji, hivyo tunawasisitiza wazazi kuwa chakula ambacho mtoto angekula nyumbani mchana ndio anakula shuleni hivyo wawachangie watoto wao na kushiriki kwenye shughuli za ujenzi miundo mbinu shulen" alisema Kaponda.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...