Search This Blog

Thursday, June 17, 2021

Ukosefu wa Elimu kwa wazazi, walezi Chanzo Cha watoto wadogo kutelekezwa


Na Baraka Messa, Songwe.

Ukosefu wa Elimu kwa Wazazi na walezi umetajwa kuwa chanzo cha Ukatili wa Mtoto na Mwanamke Wilayani Songwe Mkoani Songwe.

Hayo yamezungumzwa na Afisa Ustawi wa Jamii Songwe DC Macrina Mayage wakati wa kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama  siku ya mtoto wa Afrika kilichofanyika Ukumbi wa Ofisi ya Maendeleo Halmshauri.

Amesema wazazi wengi wamekuwa wakiwaficha watoto waliofanyiwa ukatili ,walio telelekezewa watoto pamoja na wengine kukataa kutoa ushaidi Mahakama jambo linalorudisha nyuma haki ya mtoto.

Mayage amesema kutokana na shughuli mbalimbali za kiuchumi zinazofanyika Wilayani Songwe kama uchimbaji wa madini, ufugaji, uwindaji na uvuvi vimekuwa vikipelekea ukatili wa watoto kama ndoa za utotoni, mimba za utotoni, ubakaji, utekelezwaji wa watoto chini ya miaka mitano.

Ameainisha kuwa kuanzia Julai 2020 hadi Juni 2021 jumla ya watoto 192 wamefanyiwa ukatili, wasichana wakiwa 126 na wa kiume wakiwa 66, ambapo amesema mbali na elimu  sababu nyingine zinazopelekea ukatili huo ni umaskini, na mila na desturi.

Ameongeza kuwa ni wakati sasa jamii ya Wilayani Songwe, mkoa wa Songwe na Tanzania kwa ujumla kuamka na kupinga vitendo vyovyote vinavyoashiria ukatili wa Mtoto pamoja na Mwanamke.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...