Rais wa Uganda Yoweri Museveni na mwenzake wa Jmahuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi wamezindua mradi wa ujenzi wa barabara kati ya nchi hizo mbili.
Hafla ya uzindunzi wa mradi huo ilifanyika katika mji wa mpakani wa Mpondwe wilaya ya Kasese magharibi mwa Uganda na Kasindi katika mkoa wa Kivu kaskazini mwa DRC.
Katika taarifa ya pamoja viongozi hao wawili mradi huo utaimarisha uchumi na maisha ya raia wao.
Walisistiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiana katika masuala ya usalama, kawa, biashara, uwekezaji na usimamizi wa maji ya mpakani, mafuta ya petroli na madini.

No comments:
Post a Comment