Search This Blog

Thursday, June 3, 2021

Nyota sita kuwakosa Ruvu Shooting leo

 


WAKATI kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kikiwa na kibarua cha kusaka pointi tatu leo mbele ya Ruvu Shooting kuna nyota sita ambao watakosekana katika kikosi cha leo.

Kwa mujibu wa Kocha Msaidizi, Seleman Matola ameweka wazi kwamba kuna baadhi ya nyota ambao watakosekana katika mchezo wa leo ambao utakuwa na ushindani mkubwa.

Nyota hao ambao Matola amewataja ni wawili ambao ni beki kisiki Joash Onyango pamoja na Clatous Chama.

Onyango bado anatibu majeraha aliyopata kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs huku Chama akiwa na matatizo ya kifamilia baada ya mke wake kutangulia mbele ya haki hivyo yupo Zambia.

Mbali na hao ambao amewataja Matola pia rekodi zinaonyesha kwamba nyota wao Francis Kahata hatakuwa sehemu ya kikosi cha leo kwa sababu dili lake linahusu kucheza mechi za kimataifa na Simba ilitolewa hatua ya robo fainali.

Pia kipa namba mbili Ally Salim hayupo kwenye mpango wa Gomes sawa na kiungo Ibrahim Ajibu ambaye sio chaguo la kwanza la Mfaransa huyo hivyo kuna hatihati nao pia wakaukosa mchezo wa leo.

Kiungo Jonas Mkude yeye anatajwa kuwa kwenye matatizo ya kinidhamu na alikosa mchezo uliopita dhidi ya Namungo FC wakati ubao uliposoma Namungo 1-3 Simba, Uwanja wa Majaliwa.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...