Search This Blog

Thursday, June 3, 2021

Hatima ya Sabaya na Kakoko ipo Takukuru




Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) inaendelea na uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili aliyekuwa Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Deusdedit Kakoko na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya.

Akizungumza na gazeti hili juzi, Msemaji wa Takukuru, Doreen Kapwani alisema wanaendelea na uchunguzi na wakati wowote utakapokamilika, watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

Machi 28 wakati akipokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Rais Samia Suluhu Hassan alimsimamisha kazi Kakoko kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha bandarini.

Rais Samia aliiagiza Takukuru kufuatilia suala hilo kwa sababu ripoti ya CAG ilibainisha ubadhirifu wa fedha pale bandarini na kwamba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliunda kamati iliyofanya uchunguzi na kubaini kasoro hizo na kuchukua hatua ya kuwasimamisha watendaji wachache.

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo alinukuliwa na vyombo vya habari hivi karibuni akieleza taasisi yake ilimkamata Kakoko na kumwachia kwa dhamana.

Mbungo alieleza pia uchunguzi wa tuhuma dhidi ya Kakoko ulikuwa umekamilika kwa asilimia 98 na asilimia mbili zimebaki kufanywa na CAG kisha jalada kupelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa hatua zaidi.

Mei 13, pia Rais Samia alimsimamisha kazi Sabaya ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.\

Ingawa taarifa ya Ikulu haikueleza wazi tuhuma dhidi ya Sabaya, lakini kumekuwa na malalamiko hasa ya wafanyabiashara kulazimishwa kutoa fedha kwa kiongozi huyo



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...