Mrisho Mpoto amtaka mwijaku kuwa Mzalendo kwa kumpa sapoti msanii Daimond Platinum kwenye tuzo za BET.
Sakata linaloendelea kwenye mitandao ya kijamii ni tuzoya BET ambapo Mtanzania Daimond Platinum ametajwa kuwania tuzo hizo limeibua sura mpya baada mwanamitandao maarufu na mtangazaji wa clouds Media Mwijangu kuwa gumzo baada ya kujionyesha 'live' kutompigia kura msanii huyo na kumpigia debe Burna Boy kutoka nchi nyingine.
Inajulikana moja kwa moja kuwa Mwijaku ni rafiki mkubwa wa Harmonize ambaye ni hasimu mkubwa wa Diamond
Mwijaku amekua akipiga promo ya kupigiwa kura Burna Boy ili ashinde kitendo ambacho kimewakera watu wengu kumpika na kumshauri kuwa awe mzalendo na nchi yake.
Kupitia ukurasa wa instagramu Mrisho Mpoto ameandika hivi;
"Mwijaku-Mwijaku-Mwijaku Nimekuita Mara tatu nakujua vizuri sana na najua unafahamu vizuri mno umekuwa Manager wangu kwa muda mrefu.
Najua page nyingi za watu mashuhuri zinaendeshwa na watu nikuombe chukua page yako na endesha mwenyewe.
Unachokifanya kwa Tuzo BET kwa ndugu yako mnaetoka kumoja na ni Mtanzania mwenzetu siyo sawa, kuna leo na Kesho hii ni kukosa UZALENDO na UTAIFA Ikitoea ukafanikiwa dhamira yako Utakuwa umetukosea sana wa Tanzania, nikuombe tu Aidha uache au rudi nyumbani kumenoga"
No comments:
Post a Comment