Search This Blog

Thursday, June 3, 2021

Biden kulipa kisasi dhidi ya Urusi kwa shambulizi la mtandao


Rais wa Marekani Joe Biden amesema anatafuta uwezekano wa kulipa kisasi dhidi ya Urusi baada ya serikali mjini Washington kuihusisha Moscow na shambulizi la mtandao lililoilenga kampuni kubwa ya kusindika nyama duniani ya JBS.A

kijibu swali la mwandihsi habari iwapo atamchukulia hatua rais Vladimir Putin wa Urusi ambaye amepangiwa kukutana naye mjini Geneva baadaye mwezi huu, Biden amesema serikali yake "inatafakari suala hilo kwa karibu"

Shambulizi la mtandao dhidi ya tawi la Marekani la kampuni ya kusindika nyama ya Brazil, JBS, kwa mara nyingine limezusha lawama kwamba Urusi inawahifadhi wahalifu wa mifumo ya kompyuta.Idara ya Upepelezi ya Marekani FBI ilisema jana kuwa inahusisha shambulizi hilo na majina mawili yenye mafungano na Urusi na kwamba inafanya kazi ya kuwafikisha mbele ya mkono wa sheria wahalifu hao.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...