Mkosoaji wa serikali ya Urusi Dmitry Gudkov amekamatwa na vyombo vya usalama jana na taarifa zinasema huenda atakabiliwa na kifungo jela.
Taarifa za kukamatwa kwake zimethibitishwa na baba yake mzazi aliyesema kuwa Gudkov alikamatwa baada ya msako wa polisi kwa madai ya kutolipa kodi ya nyumba tangu mwaka 2015.
Kukamatwa kwa Gudkov mwenye umri wa miaka 41 kunakuja siku moja tangu polisi ya Urusi ilipomkamata mkosoaji mwingine wa serikali Andrei Pivovarov, kwa kumshusha kutoka kwenye ndege iliyokaribia kuanza safari.
Kushikiliwa kwa Gudkov na Pivovarov ni matukio ya karibuni kabisa ya kile wakosoaji wa ikulu ya Kremlin wanakitaja kuwa kampeni ya vitisho dhidi ya wapinzani wa rais Vladimir Putin kabla ya uchaguzi wa Bunge wa mwezi Septemba.

No comments:
Post a Comment