Search This Blog

Wednesday, June 2, 2021

Erdogan aionya Marekani kabla ya mkutano na rais Biden


Rais wa Uturuki Reccip Tayyip Erdogan ameonya kuwa Marekani huenda itapoteza "rafiki muhimu" iwapo itaendelea kuinyooshea kidole cha lawama Uturuki na kuwaunga mkono wale aliowataja kuwa "magaidi". 

Akizungumza kwenye mahojiano na kituo cha televisheni ya taifa ya Uturuki Erdogan amesema iwapo Marekani ni mshirika wa kweli haipaswi kuyaunga mkono makundi ya wapiganaji ikiwemo Wakurdi wa Syria ambao Uturuki inawazingatia kuwa magaidi. 

Matamshi hayo mazito yametolewa kiasi wiki mbili kabla ya mkutano kati Erdogan na rais Joe Biden wa Marekani uliopangwa kufanyika pembezoni mwa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Kujihami NATO mjini Brussels. 

Mahusiano kati ya mataifa hayo mawili wanachama wa NATO yamepwaya kwa kiasi kikubwa tangu Biden alipoapishwa kuwa rais wa Marekani na kuchukua msimamo wa kukosoa rikodi dhaifu ya haki za bidanamu nchini Uturuki



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...