Na Timothy Itembe Mara.
MADIWANI wa halmashauri ya Tarime wameitaka halmashauri kupeleka fedha za mapato ya ndani asilimia 10 zinazokopeshwa makundi maalumu,Wanawake,Vijana na watu wenye ulemavu kwa wakati.
Diwani kata ya Kemambo,Rashidi Bogomba Chichake alisema kwenye baraza la amdiwani jana kuwa wanataka kujua vikundi vinavyokopeshwa kwa majina ikiwemo michakato ya kukopa ikoje.
"Watu wa vikundi wanaokopeshwa fedha za mapato ya ndani asilimia kumi inawezekana wanashindwa kurudiaha fedha hiyo kutokana na mazingira ya kukopeshwa yalikuwa na mazingira ya rushwa kwa hali hiyo kurudisha itawawia vingumu"alisema Chechake.
Chechake aliongeza kusema kuna haja madiwani kujua vikundi vinavyokopeshwa kwa majina kwa sababu ni haki yao na kuondokana na lawama zinazojitokeza.
Kwa upande wake diwani kata ya Itiryo,Shadarack Marwa awali alisema kuwa kiasi walichonacho cha akiba cha kukopesha makundi hayo,Wanawake,Vijana na watu wenye ulemavu kinatakiwa kubainishwa ndani ya baraza la madiwani ili wakaek wakijua.
Marwa aliongeza kuwa fedha hizo zinakuwa zinatengwa kila mwaka kutokana na makusanyo ya mapato ya ndani pia vikundi vinavyokopeshwa vinarejesha lakini madiwani hawajui ndani ya mfuko huo kuna kiasi gani chaakiba badala yake wanapokea malalamiko kutoka halmashauri kuwa vikundi havirejeshi kuna mazingira gani tata.
Naye mkurugenzi wa halmashauri ya Tarime,Apoo Tindwa alisema kuwa fedha za mikopo ya vikundi ni mchakato kwahali hiyo mchakato unaanza kwenye kata kwa hali hiyo madiwani watakuwa wanashirikishwa.
Tindwa alitaka kujua Afisa wake ambaye anatumia madaraka yake kuwaomba kitukidogo wakopeshwaji ili kumchukulia hatua za kisheria.

No comments:
Post a Comment