Search This Blog

Saturday, June 12, 2021

Burudani kutawala Mkesha wa Mwenge wa Uhuru Uwanja wa Kwaraa Mjini Babati


Na John Walter-Manyara

Mkuu wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere amesema mwenge wa Uhuru  utakimbizwa kwa kilomita 1,089.3 mkoa hapo ambapo utakukagua, kutembelea, kuona na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi 29 yenye thamani ya sh 6.6 bilioni.

Mwenge wa uhuru ambao kwa sasa upo Mkoani Manyara, katika wa wilaya ya Simanjiro  umetembelea na kukagua na kuona miradi sita ya gharama ya shilingi 239, 159, 539.10.

Mwenge wa uhuru utawasili katika wilaya ya Babati Jumapili juni 13 huku ratiba ikionyesha kuwa  kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Josephine Mwambashi  ataweka jiwe la msingi mabweni mawili shule ya sekondari Ayalagaya, kuzindua mradi wa vijana wa boda boda kwa kwa kugawa pikipiki mtaa wa Miomboni mjini Babati, kutembelea mradi wa maji Kijiji cha Imbilili, kuitembelea klabu ya wapinga rushwa shule ya msingi kibaoni.

Pia Kiongozi huyo atatembelea na kuona mradi wa TEHAMA kituo cha Afya Magugu na kuweka jiwe la msingi hospitali ya wilaya ya Babati katika kata ya Mwada kisha kuelekea katika uwanja wa Kwaraa Mjini Babati ambapo Mwenge huo utakesha uwanjani hapo.

Katibu tawala wilaya ya Babati Halfan Matipula na mratibu wa mwenge Babati Mjini Fabian Manda wamesema burudani mbalimbali zitakuwepo kwenye mkesha wa mwenge katika uwanja wa Kwaraa huku ulinzi na usalama ukihimarishwa.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni Tehama ni msingi wa Taifa endelevu itumie kwa usahihi na uwajibikaji.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...