Search This Blog

Tuesday, June 8, 2021

Kocha wa Smba asepa Bongo


 DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amekwea pipa na kuibukia nchini Ufaransa kwa ajili ya mapumziko mafupi.

Raia huyo wa Ufaransa ambaye ameongoza kikosi hicho mpaka kuishia hatua ya robo fainali katika Ligi ya Mabingwa Afrika alikwea pipa Juni 5.

Ikumbukwe kuwa alijiunga na Simba Januari 24 akichukua mikoba ya Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji na alisepa na Ndege ya Shiriki la KLM.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa:" Timu kwa jumla ina mapumziko hadi Juni 8 mwaka huu ndio tutarejea tena  kazini," .

Gomes anatarajiwa kurejea Bongo Juni 11 kuendelea na kazi yake.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...