Search This Blog

Sunday, June 6, 2021

Huyu ndiye TB Joshua kuzaliwa hadi kufariki saa chache baada ya Ibada


Temitope Balogun Joshua, maarufu TB Joshua, alizaliwa tarehe 12 mwezi Juni 1963 katika ya mji wa Arigidi huko Aoko kaskazini mashariki mwa jimbo la Kusini magharibi mwa Nigeria.

Utotoni alitambulika kwa jina la Balogun Francis na alianza kupata elimu ya msingi katika shule ya Kianglikana ya St. Stephen huko Arigidi Akoko, Nigeria, kati ya mwaka 1971 na 1977, lakini alishindwa kumaliza mwaka mmoja wa elimu yake ya sekondari.

Shuleni alijulikana kama "mchungaji mdogo" kwa sababu ya kupenda kwake Biblia. Alifanya kazi za kawaida baada ya kumaliza shule, ikiwa ni pamoja na kubeba taka kwenye shamba la kuku.

Alijaribu kujiunga na jeshi la Nigeria, lakini alishindwa kwa sababu ya kuharibika kwa treni na kukwama wakati akielekea kwenye chuo cha kijeshi.

Umaarufu wake ulisambaa kote Afrika na Amerika Kusini, na kutajwa na majarida ya Pan-Africa, The Africa Report na New African Magazine, kama mmoja kati ya watu 50 wenye ushawishi mkubwa barani Afrika.

Kuanzia mwaka 2011, kulingana na jarida la Forbes, TB Joshua alikuwa mchungaji wa tatu kwa utajiri duniani, ingawa baadaye taarifa hiyo ilikataliwa katika taarifa ya kanisa lake.

T.B Joshua ni mwanzilishi wa Kanisa la 'SCOAN' The Synagogue Church of All Nations, kanisa kuu la Kikristo ambalo linaendesha kituo maarufu cha runinga cha Emmanuel TV pale Jijini Lagos.

Muhubiri huyo maarufu kutoka nchini Nigeria amefariki Jumamosi ya Juni 5, 2021 nyumbani kwake Jijini Lagos, muda mfupi baada ya kumaliza kutoa mafundisho yake.

Aidha taarifa ya kifo chake ilisema: Mungu amechukua maisha ya muhudumu wake TB Joshua kulingana na uwezo wake. Amefariki akimuhudumia Mungu.

Taarifa hiyo imetaja sura moja katika biblia inayosema : Mungu muweza hawezi kufanya lolote bila kutoa mipango yake kwa watume wako. " - Amos 3: 7

Siku ya Jumamosi tarahe 5 Juni 2021, mtume TB Joshua alizungumza katika mkutano wa runinga ya Emmanuel.

''Kila kitu kina wakati wake - tunapokuja hapa na kuomba na tutarudi nyumbani baada ya utumwa''.

TB Joshua alikuwa mmoja ya wahubiri maarufu ambapo alijulikana kwa kutabiri matukio yajayo ambayo wengi waliona kama uingiliaji wa kazi ya Mungu.

Mwaka 2014, Muhubiri huyo alikosolewa nchini Nigeria baada ya upande mmoja wa paa la kanisa lake nchini humo kuanguka na kuwaua takriban watu 116.

TB Joshua ana makanisa mengi katika mataifa tofauti barani Afrika na Marekani ya kusini.

R.I.P TB JOSHUA.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...