Serikali ya Nigeria imesema itawachukulia hatua za kisheriawatu watakaobainika kukiuka katazo la matumizi ya mtandao wa kijamii wa Twitter.
Juni 4, 2021 Nigeria ilitangaza kusitisha matumizi ya mtandao huo.
Baada ya Twitter kufuta ujumbe uliowekwa na Rais wa nchi hiyo, Muhammadu Buhari kwa kukiuka sheria za mtandao huo.
Msemaji wa Serikali ya Nigeria amesema kuondolewa kwa ujumbe huo kulikatisha tamaa lakini sio sababu pekee ya kusimamishwa kwa muda kwa matumizi ya mtandao huo.

No comments:
Post a Comment