Search This Blog

Sunday, June 6, 2021

CCM Kiwangwa yahimiza mikutano ya mapato na matumizi


Na Omary Mngindo, Kiwangwa.

CHAMA Cha Mapinduzi CCM Kata ya Kiwangwa Halmashauri ya Chalinze wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, imewataka viongozi wa Serikali za Vijiji kuitisha mikutano ya kuwasomea mapato na matumizi.

Katibu wa chama hicho katani hapa Rashid Kufuru aliyasema hayo mwishoni mwa wiki, akizungumza na Waandishi wa habari ambapo alisema kuwa wamefanya ziara ya kutembelea vijiji na vitongoji kuzungumza na wenyeviti kuhusiana na mikutano hiyo.

Alielezea kwamba Kamati yao iliamua kuandaa ziara hiyo, ambapo mbali ya kuhamasisha mikutano pia kutoa semina elekezi kwa viongozi hao ili kila mmoja atambue majukumu na mipaka ya kazi yake kwa lengo la kuhepusha migongano.

"Ziara yetu iliyoandaliwa na Kamati ya siasa ya chama chetu ngazi ya Kata imelenga kuwaelimisha viongozi wetu wote ambao wametokana na chama chetu kikubwa kuandaa mikutano ya kuwasomea mapato na matumizi wananchi wao, ili kuondoa malalamiko," alisema Kufuru.

Aisha aligusia changmoto ya wafugaji kuchunga mifugo yao kwenye mashamba,  jambo linalosababisha migongano mkubwa, huku wananchi wakulima imani na viongozi wao jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wao.

Mmoja wa wenyeviti wa Kitongoji cha kwa-Mbwela Omary Koyo alisema kwamba ziara hiyo imekuwa na mafanikio, kwani wamepata elimu ya kutosha hivyo kuwaongezea uelewa wa namna gani wanavyotakiwa kutekeleza majukumu yao kwa wanaowaongoza.

"Binafsi nimeipokea kwa moyo mkunjufu ziara ya Kamati yetu ya siasa kata, kwani kuna mambo mingi nimejifunza kupitia ziara iliyofanyika, tumeagizwa mambo kadhaa ya kuyatekeleza ikiwemo kuwasomea mapato na matumizi, kusikiliza kwa wakati kero zao pia migongano ya wakulima na wafugaji," alisema Koyo. 

Alimalizia kwa kusema kwamba atashirikiana vyema pamoja na wajumbe wanaounda serikali yao, huku akiwataka wananchi kuwapatia ushirikiano viongozi wao ili kutekelezwa ipasavyo majukumu yanayowakabili kwa maslahi ya wananchi wa kwa-Mbwela.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...