Makamu wa Rais wa Marekani (USA) Kamala Harris, alitangaza kwamba wahamiaji wa Guatemala wanaoingia nchini kinyume cha sheria watarudishwa nchini kwao.
Wakati wa ziara yake ya kwanza ya nje ya nchi aliyoitekeleza huko Guatemala, Harris alipokelewa na Rais wa Guatemala Alejandro Giammattei katika Ikulu ya Kitaifa ya Utamaduni.
Harris na Giammattei walifanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari baada ya mkutano kati ya wajumbe.
Giammattei alisisitiza kuwa shida ya wahamiaji inayoongezeka hivi karibuni inasababisha matatizo makubwa na kusema,
"Kuna mambo mengi ambayo yanahitaji tushirikiane. Watu wanahitaji kupata fursa za kuishi hapa na sio kuzitafuta mahali pengine."
Kwa upande mwingine, Harris alisema kwamba alifanya ziara hii Guatemala kujadili maswala ya uhamiaji haramu, vurugu na ufisadi.
Kamala Harris alionya kuwa wahamiaji wa Guatemala wanaoingia Marekani kinyume cha sheria watarudishwa nchini mwao.

No comments:
Post a Comment