Search This Blog

Tuesday, June 8, 2021

Nyumba ya vilipuzi ya Al-Shabaab yalipuka na kusababisha wanachama wasiopungua 60 kufariki


Wanachama wasiopungua 60 wa shirika la kigaidi wameripotiwa kufariki kwebnye mlipuko uliotokea katika nyumba iliyojaa vilipuzi inayomilikiwa na shirika la kigaidi la Al-Shabab nchini Somalia.

Wakitoa taarifa kwenye redio ya jeshi la Somalia, maafisa wa jeshi walisema kwamba wanachama wasiopungua 60 waliuawa kwenye mlipuko uliotokea katika nyumba ambayo wataalam wa mabomu na wanamgambo wa shirika hilo walikuwemo katika mji wa Ala-Futow mkoa wa Lower Shabel.

Mwanamke mmoja na mtoto ambaye aliishi katika maeneo ya jirani walipoteza maisha kutokana na mlipuko huo uliotokea kwenye nyumba ya vyumba 11 ambapo vifaa vya kutengenezea bomu vilikuwa vikihifadhiwa.

Maafisa wa jeshi walisema kwamba mmoja wa wanachama 6 wa kigeni waliokufa kutokana na mlipuko huo alikuwa Ahmed Sharif, ambaye alikwenda eneo hilo kutoka Afghanistan.

Jeshi la Somalia lilitangaza hapo jana kuwa zaidi ya wanachama 100 wa shirika hilo waliangamizwa katika wiki 3 zilizopita kwenye operesheni ya kijeshi iliyozinduliwa dhidi ya shirika hilo.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...