Katika mkutano wake wa kwanza tangu kuondoka katika Ikulu ya White House, aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump jana jumamosi alishtumu sera za uhamiaji za utawala wa Biden na kuwahimiza wafuasi wake kuwasaidia wabunge wa chama cha Republican kuchukuwa wingi wa viti bungeni.
Akihutubia maelfu ya wafuasi wake katika jimbo la Ohio nchini humo, Trump alitaja orodha ya malalamiko yake ya kila mara huku akishtumu uchaguzi wa nchi hiyo na hasa kuangazia idadi inayoongezeka ya wahamiaji wanaovuka kuingia nchini Marekani kupitia mpaka wake wa Kusini.
Huku Trump akiwa ametoa hotuba katika hafla za chama cha Republican tangu kuondolewa madarakani na rais Joe Biden wa chama cha Democratic, mkutano huo katika jimbo alilopata wingi wa kura katika uchaguzi wa mwaka 2020 unaadhimisha kurejea tena kwa aina ya mikutano huru mikubwa ambayo imekuwa muhimu katika kudumisha uungwaji mkono katika ngome yake.

No comments:
Post a Comment