Na katika michezo, Italia iliifunga Austria mabao mawili kwa moja katika muda wa ziada jana jusiku uwanjani Wembley na kufuzu hatua ya robo fainali ya Euro 2020 na kujiunga na Denmark ambayo ilipenya kwa kuichabanga Wales mabao manne kwa sifuri.
Italia, inayoongozwa na kocha Roberto Mancini na ambayo inapigiwa upatu kufanya vyema katika mashindano haya baada ya mchezo mzuri katika hatua ya makundi, ililazimika kuufanyia kazi kubwa ushindi wake. Italia sasa itakutana na mshindi wa mechi ya leo kati ya Ubelgiji na Ureno.
Nayo Denmark itacheza na mshindi wa mechi kati ya Uholanzi na Jamhuri ya Czech.

No comments:
Post a Comment