Search This Blog

Sunday, June 27, 2021

Waziri wa afya wa Uingereza ajiuzulu kwa kuvunja sheria za corona

 


Waziri wa afya wa Uingereza Matt Hancock amejiuzulu. Hancock amejiuzulu baada ya kuvunja sheria ya kuthibiti kuenea kwa virusi vya corona kwa kuweka umbali wa mtu mmoja hadi mwingine akiwa na msaidizi wake mkuu Gina Coladangelo anayedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi naye. 

Gazeti la The Sun lilichapisha picha zilizoonekana kumuonesha Hancock na Coladangelo wakibusiana katika ofisi moja ya wizara hiyo ya afya. 

Katika barua yake ya kujiuzulu kwa waziri mkuu Boris Johnson, Hancock alisema kuwa serikali ina wajibu kwa watu wake ambao wamejitolea pakubwa katika janga la virusi vya corona, kuwa waaminifu kwao wakati imewakosea.

Hancock aliongeza kuwa anataka kusisitiza ombi lake la msamaha kwa kuvunja muongozo na kuiomba radhi familia na wapendwa wake kwa tukio hilo na kwamba anahitaji kuwa na watoto wake kwa wakati huu.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...