Search This Blog

Friday, June 4, 2021

Dereva aliyesababisha ajali Shinyanga akamatwa Nzega


Baada ya ajali ya basi la Kampuni ya Classic iliyotokea hapo juzi eneo la Didia Wilayani Shinyanga na kusababisha vifo vya watu wanne wakiwemo wanafunzi watatu wa Chuo Kikuu Bugema Jijini Kampala, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo ametembelea eneo la tukio sambamba na kuwajulia hali majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga kisha akawataka waendesha vyombo vya moto kuwa waangalifu wawapo barabarani.

Aidha kwa upande wake kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga akizungumza juu ya hatua zilizochukuliwa hadi sasa baada ya dereva wa basi hilo kukimbia, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Debora Magiligimba amesema kuwa tayari mtuhumiwa huyo amekatwa wilayani Nzega mkoani Tabora



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...