Mfungwa wa Senegal anayefahamika kama Mtoro sugu wa jela , Baye Modou Fall ambaye alitoroka Jumamosi kutoka gerezani katika mji mkuu Dakar amekamatwa tena.
Ilikuwa ni mara ya 12 akitoroka kutoka kwenye magereza nchini, vimeripoti vyombo vya habari nchini humo.
Alikamatwa katika eneo la Moussala mashariki mwa nchi karibu na mpaka nan chi jirani ya Mali, msemaji wa jeshi la Senegal aliliambia Shirika la habari la AFP.
Mfungwa huyo mwenye umri wa miaka 32, ambaye anafahamika kama"mtoro sugu " Jumatatu aliiambia televisheni nchini humo kwamba alikuwa ametoroka kwasababu mchakato wa sheria ulikuwa unachukua muda mrefu sana na alitoroka kupitia ukuta wa gereza akitumia.
Alielezea jinsi alivyotoroka kutoka gerezani kwa kuvunja kifaa kinachoingiza hewa ndani ya mahabusu na kupanda juu ya ukuta akitumia kamba.
Maafisa wanachunguza kama kulikuwa na mtu aliyemsaidia katika kutoroka.

No comments:
Post a Comment