Search This Blog

Friday, June 4, 2021

Netanyahu awataka wabunge wa Israel kuipinga serikali mpya


Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amewatolea wito wabunge waipinge serikali mpya ya mseto itakayoongozwa na Naftali Bennett. 

Netanyahu amemkosoa mrithi wake mtarajiwa akiandika katika ukurasa wake wa twitter kwamba Bennett ameliuza eneo la Negev kwa chama cha waarabu cha Ra'am, ambacho kitajiunga na serikali ya mseto kwa mara ya kwanza, pamoja na jangwa la Negev kusini mwa Israel.

 Inaripotiwa serikali ya mseto inajumuisha kipengee kinachositisha uvunjaji wa majengo yaliyojengwa kwa njia isiyo halali katika jangwa hilo, hali inayovitia wasiwasi vijiji vya Bedouin.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...