Search This Blog

Friday, June 4, 2021

BASATA yampongeza Diamond kuwania tuzo za BET

 


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)  limempongeza msanii Diamond Platnumz kwa kufanikiwa kutajwa kuwania tuzo za Muziki za BET za mwaka 2021 katika kipengele cha "Best International Act" (msanii aliyefanya vizuri kimataifa).

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Juni 3, 2021 na kaimu katibu mtendaji wa baraza hilo, Matiko Mniko imeeleza hayo ni mafanikio makubwa katika maendeleo ya sanaa na sio kwa Diamond pekee, bali ni kwa tasnia nzima ya mziki wa Tanzani.

Kaimu katibu mtendaji huyo ametoa wito kwa wadau wa sanaa na wananchi wote kwa ujumla walio ndani na nje ya nchi kumuunga mkono msanii wetu, ili afanikiwe kutwaa tuzo hiyo.

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Mwezi huu, Tarehe 27 huko Los Angeles, nchini Marekani.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...