Wanajeshi wa jeshi la Sudan wamekamatwa na watashtakiwa wakihusishwa na mauaji ya waandamanaji wawili katika mji mkuu Khartoum, wiki iliyopita.
Mkuu wa baraza la mpito nchini humo, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, ameamuru uchunguzi kuhusu mauaji ya siku ya Jumanne yaliyotokea nje ya makao makuu ya jeshi mjini Khartoum.
Imechukua chini ya wiki moja kwa jeshi la Sudan kuchunguza mauaji ya waandamanaji wawili.
Lakini watu wengi nchini Sudan wana ghadhabu wakidai kuwa bado hakuna haki kwa kwa ukatili mkubwa zaidi ambao ulitokea karibu miaka miwili iliyopita.
Wakati huo waandamanaji walipotaka kurudi kwa utawala wa raia kufuatia kupinduliwa kwa Rais Omar al Bashir, wanajeshi walifyatua risasi. takribani watu 128 walifariki.

No comments:
Post a Comment