Watu wenye silaha wamefanya shambulizi na kuwateka nyara watoto kadhaa kutoka shule moja ya kiislamu iliyopo kwenye jimbo la Niger katikati mwa Nigeria.
Serikali ya jimbo hilo imesema watoto 200 walikuwepo shuleni wakati wa uvamizi huo lakini idadi kamili ya wanafunzi waliochukuliwa mateka bado haijulikani.
Msemaji wa polisi ya jimbo Niger Waisu Abiodun amesema washambuliaji waliwasili eneo la shule kwa pikipiki na kuanza kufyetua hovyo risasi zilizosababisha kifo cha mkaazi mmoja na kumjeruhi mwingine.
Mmoja wa maafisa wa shule hiyo amesema awali washambuliaji waliwateka nyara watoto 100 lakini baadaye waliwarudisha wale wenye umri kati ya miaka 4 hadi 12.
Kwa muda mrefu sasa makundi ya watu wenye silaha yanaendesha ukatili kaskazini magharibi mwa Nigeria kwa kufanya uporaji wa mali, mifugo na kuteka watu nyara.

No comments:
Post a Comment