Search This Blog

Monday, May 31, 2021

Watu 177 mbaroni kwa uhalifu mbalimbali Mara


Na Timothy Itembe Mara.

Watu 177 wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa kipolisi Tarime Rorya kwa makosa mbalimbali ya kiuhalifu ikiwemo kuingia nchini bila kipali.

Akiongea na waandishi wa habari kamanda mkoa wa kipolisi Tarime Rorya,William Mkonda aliwaambia kuwa katika msako unaoendelea wa Jeshi la polisi wamefanikiwa kuwakamata watu 177 kwa matukio tofauti tofauti ikiwemo kuingia nchiuni bila kibali.

"Katika Oporesheni inayoendelea Jeshi la polisi Tarime/Rorya wamefanikiwa kukamata watuhumiwa 177 kutokana na makosa mbalimbali kupatikana kwa gongo(pombe haramu) lita 741 pamoja na mitambo mitatu na watuhumiwa 44 walikamatwa,kukamatwa kwa pikipiki 16 na wizi ambapo watuhumiwa 16,walikamatwa kwa wizi wa mifugo 17 na Ng'ombe 18 kuokolewa,kupatikana kwa Bangi kilo 403.9 n watuhumiwa 20,kupatikana kwa mirungi kilo 40 na watuhumiwa 4 walikamatwa,kukamatwa,kungia nchini bila kibali ambapo watuhumiwa 6 walikamatwa na kukamatwa kwa watuhumiwa 70 na makosa ya unyang'anyi'uvunjifu na wizi  pamoja na vifaa vya kuvunjia"alisema Mkonda.

Jeshi la polisi Tarime'Rorya limejipanga vizuri kukabiliana na uhalifu na matishio ya aina yoyote bila kuwa na mhali na mtu yeyote atakaye vunja au kukiuka sheria za nchi aliongeza kusema Mkonda.

Wakati huo huo mkuu wa kikosi cha usalama barabarani(RTO) Shaal Shaal alisema jeshi la polisi wanaendelea kutoa elimu ya uraia pamoja na ya usalama Barabarani kwa watumiaji ili kupunguza vifo vitokanavyo na Ajali barabarani kama sio kuisha kabisa.

Shaal aliongeza kuwa katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Machi Mei ajali za pikipiki zilikuwa 3 na majeruhi 2 idadi ya ajali za magari zilikuwa 8 idadi ya vifo vitokanavyo na magari 4 na majeruhi 15.

Mkuu huyo alimaliza kwa kusema kuwa polisi wanawawekea madereva alama katika leseni zao kwa kupunguza point na kuwafungia leseni zao kwa madereva wanaofanya makosa makubwa ambayo ni hatarishi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...