Na, Baraka Messa, Songwe.
KAIMU mkuu wa Wilaya ya Ileje ambaye pia ni mkuu wa Wilaya ya Mbozi John Palingo amevipongeza vyombo vya habari kwakuibua changamoto mbalimbali za ukatili wa watoto na awajawazito ambavyo vimekisir mkoani Songwe.
Kaimu mkuu wa Wilaya ameyazungumza hayo Jana katika siku ya maazimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari mkoa wa Songwe yaliyofanyika mei 8, wilayani Ileje huku wakialikwa wadau mbalimbali kujadili changamoto na umhimu wa vyombo vya habari katika jamii.
Alisema pamoja na mkoa wa Songwe kukumbwa na changamoto za unyanyasaji akina mama wajawazito,ukatili wa watoto wadogo na utelekezaji watoto wadogo wenye chini ya umri wa miaka nane ,vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti mara kwa mara na kuisaidia serikali kuchukua hatua kali kwa baadhi ya wahusika.
Palingo alisema ushirikiano wa Serikali dhidi ya vyombo vya habari utaendelea kuimalika kwa kuwa waandishi wa habari wanasaidia kwa kiasi kikubwa kumlika changamoto zilizopo kwenye jamii na kuisaidia serikali kuzitatua haraka.
“Tathinia ya habari ni mhimili wa nne wa dola baada ya Serikali,Binge na mahakama hivyo wananchi wanahaki ya kupata mawasiliano, hivyo tunaomba kaibueni changamoto za wananchi hasa vijijini ili akina mama wanaotelekezwa waweze kusikia haki zao na kujua sehemu kutatuliwa changamoto zao” alisema Palingo.
Naye Roderick Sengela afisa Maendeleo ya jamii alisema katika Wilaya ya Ileje Kuna changamoto kubwa za mimba za utotoni na unyanyasaji wa kijinsia ambao hufumbiwa macho na jamii zinazowazunguka ,hivyo amevitaka vyombo vya habari kuibua hayo ili kuvikomesha vitendo hivyo.
Alisema masoko yanayofanyika usiku katika mkoa wa Songwe yamekuwa chanzo cha kuibuka kwa ukatili wa kijinsia na kutokea mimba za utotoni na kutelekezwa watoto pindi wanapozaliwa .
Kwa upande wao waandishi wa habari wamewataka viongozi wa ngazi za chini kujitahidi kutoa ushirikiano pindi waandishi wa habari wanapotaka kuibua changamoto mbalimbali zinazozikumba jamii husika.
Mwandishi wa ITV mkoa wa Songwe Gabriel Kandonga alisema muda mwingine madiwani wamekuwa wakizuia kuyaibua maovu mbalimbali kwenye kata zao kwa kuhofia kukosana na wananchi ambao ni wapiga kura wao na kupelekea maovu kuongezeka.
“Tunawaomba wanasiasa hasa madiwani kuacha kuwakumbatia watenda maovu ya kuwafanyia ukatili watoto kwa kuhofia kutopigiwa kura kipindi cha uchaguzi, ili kukomesha maovu haya tunaomba tushirikiane ikiwa ni pamoja na kuviacha vyombo vya habari kufanya kazi ya kuibua maovu yaliyo katika jamii” alisema Kandonga.
Mwandishi na mtangazaji wa Ileje FM Asifiwe Minga alisema changamoto nyingine iliyopo vijijini ni wananchi kuogopa vyombo vya habari, pindi wanapotaka ushirikiano kwao baada ya changamoto kutokea.
Alisema ni vema viongozi wa maeneo ya vijijini ambako unyanyasaji umekithiri waanze kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umhimu wa vyombo vya habari katika kuwasaidia kufikisha changamoto zao sehemu kwa wahusika ambao ni viongozi wa ngazi za juu.

No comments:
Post a Comment