Search This Blog

Monday, May 10, 2021

Paulina Gekul afuturisha wakazi wa Babati

 




Na John Walter-Babati.

Naibu waziri wa Habari, Sanaa,Burudani na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Babati mjini Paulina Philipo Gekul  amejumuika na mamia ya waislamu katika Iftari aliyoiandaa na kufanyika katika chuo cha uhasibu Babati.


Katika hafla hiyo viongozi mbali mbali wa Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) walihudhuria, akiwemo mwenyekiti wa ccm  mji wa Babati Elizabeth Marley, katibu Feisal Dauda,Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya mji wa Babati Fortunatus Fwema na Menyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Babati Abrahaman Kololi.

 Wengine ni pamoja na Katibu tawala mkoa wa Manyara Musa Missaile, katibu tawala wilaya ya Babati Hassan Matipula.

Akitoa shukran kwa waalikwa, Gekul  amesema amefarikijika sana na muitikio wa waumini hao, huku akieleza upendo alionao kwa wananchi wa Babati ni mkubwa ndio maana ameamua kukutana nao na kufuturu pamoja licha ya  vikao vya Bunge na majukumu mengine ya kitaifa.

Aidha, Gekul alitumia fursa hiyo kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwawezesha waumini hao kutekeleza vyema ibada hiyo muhimu ya funga, na kusema kukutana kwao huko ni jambo la kheri.


Nae Shehe Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Sheikh Mohamedi  Kadidi amemuombea dua Naibu waziri Paulina Gekul pamoja na kumtakia kheri nyingi kwa Mwenyezi Mungu kwa maandalizi mazuri ya iftari hiyo.

Alitumia fursa hiyo kumtakia rehema yeye na familia yake , akibainisha wema mkubwa aliowafanyia waumini waliotikia mwaliko wake.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...