Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Anthonio Guterres amesema anaamini kwamba Israel inalazimika kujizuia kutumia nguvu na kuheshimu haki ya watu kukusanyika kwa amani.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema hayo kwenye taarifa wakati wasiwasi ukizidi kuongezeka katika eneo la msikiti wa al Aqsa, Jerusalem Mashariki.
Dujarric amesema katibu mkuu ameelezea wasiwasi wake juu ya machafuko yanayoendelea katika eneo linalokaliwa kimabavu la Jerusalem Mashariki, pamoja na uwezekano wa familia za Wapalestina kuondolewa kwenye makazi yao.
Amesema katibu mkuu huyo amewaiomba Israel kusitisha mpango wa kuvunja na kuwaondoa wakazi hao, na kuongeza kuwa hadhi ya maeneo matakatafu ni lazima iendelelezwe na kuheshimiwa.

No comments:
Post a Comment