Na Hamisi Nasri, Masasi.
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa( TAKUKURU) wilayani Masasi mkoani Mtwara imewafikisha Mahakamani katika mahakama ya wilaya ya Masasi viongozi wawili wa Chama Cha Msingi Mkululu (AMCOS) wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.
Viongozi hao ambao wamefikishwa katika mahakama hiyo ni Rashidi Hamisi ambaye ni mwenyekiti wa Chama hicho cha Msingi na katibu wake, Omari Timamu.
Kesi hiyo namba 8 ya mwaka 2021 imesomwa mwishoni mwa wiki katika mahakama hiyo mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo ya wilaya ya Masasi, Bastita Kashusha.
Akisoma kesi hiyo mbele ya mahakama hiyo, mwendesha mashtaka wa Takukuru wilaya ya Masasi, Charles Mtungila alidai mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.
Alidai kuwa kosa la kwanza ni kutumia nyaraka za uongo kwa lengo la kumdanganya mwaajili.
Mwendesha huyo wa mashtaka wa Takukuru alidai kuwa kosa la pili ni kujipatia fedha shilingi milioni tatu kwa udaganyanyifu.
Watuhumiwa hao wawili walikana mashtaka yao na kwamba mahakama iliwataka washtakiwa hao kuweka bondi ya maneno ya shilingi milioni tatu kila mmoja ili kuweza kupata
Kesi hiyo imeaharishwa hadi tarehe 21 Mei mwaka 2021 itakapo somwa tena

No comments:
Post a Comment