Search This Blog

Tuesday, May 11, 2021

Vikosi vya Misri na Ufaransa vyaendesha zoezi la pamoja la kijeshi katika Bahari ya Shamu

Vikosi vya Wanamaji wa Misri na Ufaransa vilitekeleza zoezi la pamoja la kijeshi la "2021 Ramses" katika Bahari ya Shamu.

Msemaji wa Jeshi la Misri Kanali Tamir ar-Rifai alisema kwenye ukurasa wake rasmi wa Facebook kwamba meli ya kivita ya "Sejem al-Fatih" kutoka Jeshi la Wanamaji la Misri, na meli ya kivita ya "Charles de Gaulle" kutoka Jeshi la Wanamaji la Ufaransa, pamoja na ndege nyingi za kivita na vikosi vya majini walishiriki katika zoezi hilo.

Rifai alielezea kuwa zoezi hilo lilijumuisha mafunzo mengi ya pamoja ambayo yalinufaisha pande zote mbili.

Kwa upande mwingine, Rifai alibaini kuwa wakati wa zoezi la pamoja la kijeshi la "2021 Ramses", zoezi la pamoja la anga pia lilifanyika katika kituo kisichojulikana cha Misri.

Katika taarifa hiyo, ilielezwa kuwa zoezi hili liliendeshwa ndani ya wigo wa ushirikiano kati ya vikosi vya jeshi vya Misri na Ufaransa, kwa maslahi ya pamoja ya nchi hizo mbili na juhudi zao za kufikia utulivu katika eneo hilo.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...