Search This Blog

Tuesday, May 11, 2021

Hamas yafyatua maroketi ya nadra kuelekea Israel

 


Kundi la wanamgambo la Hamas jana lilifyatua maroketi ambayo ni nadra kuelekea Jerusalem baada ya mamia ya Wapalestina kuumuizwa kufuatia makabiliano na polisi wa Israel kwenye eneo la msikiti wa al- Aqsa. 

Hali ya wasiwasi imezidi kuongezeka kwenye mji huo mtakatifu, na kutishia kuibuka kwa vita kamili. Israel ilijibu kwa mashambulizi ya angani kote katika eneo la Ukanda wa Gaza ambako watu 20, miongoni mwao watoto tisa waliuawa. 

Zaidi ya Wapalestina 700 wamejeruhiwa walipokabiliana na polisi na 500 wanapatiwa matibabu. Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amekutana na maafisa wa ngazi za juu wa usalama jana na kuonya makabiliano hayo yanaweza kuendelea licha ya miito ya kuyasitisha kutoka kwa Marekani, Ulaya na kwingineko. 

Amesema makundi ya kigadi ya Gaza yamevuka mstari mwekundu na kuongeza yoyote anayewashambulia atajibiwa kwa mashambulizi makali.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...