Search This Blog

Friday, May 21, 2021

Umoja wa Afrika wataka viongozi wa kijeshi na kiraia Chad kugawana madaraka


Umoja wa Afrika umewatolea mwito viongozi wa kijeshi na wa kiraia nchini Chad kugawana madarana hadi pale uchaguzi utakapoandaliwa.

 Wito huo unajiri baada ya jeshi kuchukua uongozi wa taifa hilo kufuatia kifo cha Rais Idriss Deby mwezi uliopita. 

Umoja wa Afrika ulirudia miito yake ya awali kutaka uongozi wa kiraia wakati wa mpito, miezi 18 baada ya uchaguzi, na kuongeza kuwa jeshi linaweza kuendelea kusimamia masuala ya kiusalama baada likiongozwa na Mahat, mwanaye marehemu Deby. 

Kupitia taarifa, Baraza la Usalama na Amani la Umoja wa Afrika limetilia mkazo haja ya kuwepo mchakato jumuishi na makubaliano ya pamoja ya mpito utakaoongozwa na viongozi wa kiraia, na kuwe na majukumu bayana ya serikali ya mpito na ya Baraza la Mpito la Kijeshi (CMT). 

Msemaji wa CMT amesema ameyakaribisha mapendekezo hayo ya Umoja wa Afrika. Marehamu Idriss Deby aliitawala Chad, nchi muhimu kwa Ufaransa na nchi nyingine za magharibi katika vita dhidi ya wanamgambo wenye itikadi kali za Kiislamu kwa miaka 30 iliyopita. 

Kifo chake kilitokea alipowatembelea wanajeshi wake wanaopambana na waasi kaskazini mwa nchi hiyo hali iliyozusha hofu ya uwezo wa kanda hiyo kutumbukia katika msukosuko.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...