Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) liliripoti kuwa usafirishaji wa chanjo za corona (Covid-19) kwa bara la Afrika umepungua kasi.
Mkurugenzi wa WHO barani Afrika, Dk. Matshidiso Moeti aliwaambia waandishi wa habari kwamba kupungua kwa kasi ya usambazaji wa chanjo kunasababishwa na kuenea kwa haraka kwa janga hilo India, ambayo pia ni kati ya nchi zinazozalisha chanjo.
Moeti aliarifu kuwa bara lilikuwa likitarajia kupokea dozi milioni 66 za chanjo chini ya Mpango wa Usambazaji wa Ulimwenguni (COVAX) kati ya Februari-Mei, lakini dozi milioni 18 pekee ndizo zilizofika.
Akifahamisha kuwa kuna nia na shinikizo kubwa kwa chanjo hiyo kuzalishwa Afrika, Moeti alisisitiza hii inaweza kuwa suluhisho kudumu katika muda wa kati na muda mrefu.
Akisema kuwa kuna dhuluma katika utoaji wa chanjo kati ya nchi barani, Moeti pia alisema,
"Wakati Ushelisheli ilitoa chanjo kwa asilimia 67 ya idadi ya watu, nchi 14 za Kiafrika hazijaweza kutoa chanjo hata kwa asilimia 1 ya idadi ya watu na nchi 4 hazijaanza kabisa kutoa chanjo."
Ingawa kesi za Covid-19 zilipungua kote Afrika, zilionekana kuongezeka katika nchi 7 ambazo ni Benin, Eritrea, Eswatini, Liberia, Nigeria, Sierra Leone na Jamhuri ya Afrika Kusini.
Wakati idadi ya kesi barani Afrika ilizidi 4,760,000, idadi ya watu waliopoteza maisha ilizidi 127,000.

No comments:
Post a Comment