Rais Uhuru Kenyatta ameongoza hafla ya kuapishwa kwa Martha Koome kama jaji mkuu.
Koome amekula kiapo cha utekelezaji wa kazi yake kwa uadilifu katika Ikulu ya Nairobi, mjini Nairobi.
Kiapo hicho kilitekelezwa na Msajili Mkuu wa Mahakama Anne Amadi.
Akizungumza Rais Uhuru Kenyatta baada ya kuapishwa kuwa jaji mkuu Martha Koome, amesema imekuwa furaha yake kuwa rais wa kwanza kumuapisha Jaji Mkuu mpya wa kwanza mwanamke nchini humo.
Jaji Koome aliyekuwa akihudumu katika mahakama ya rufaa amekuwa katika nyanja hiyo kwa miaka 33 na anachukua uongozi kutoka kwa David Maraga ambaye alistaafu mwaka jana na ataongoza idara ya mahakama kwa kipindi cha miaka 10.
Rais wa Mahakama ya Rufaa William Ouko pia naye alikula kiapo katika hafla hiyo kuhudumu kama jaji katika mahakama ya juu zaidi nchini Kenya.
No comments:
Post a Comment