Nchi za Umoja wa Ulaya zimefikia makubaliano ya kuwa na cheti cha kidijitali cha COVID-19 kuwezesha usafiri ndani ya Ulaya.
Makubaliano hayo yatamruhusu mtu yeyote anayeishi miongoni mwa nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya kupata cheti cha kidijitali cha afya ifikapo mwisho wa mwezi Juni.
Cheti hicho kitakuwa na maelezo kama mtu amechanjwa dhidi ya COVID-19, na pia matokeo ya vipimo vyake vya maambukizi ya virusi vya corona au ikiwa amepona endapo aliugua COVID-19.
Stella Kyriades, kamishna wa afya wa Umoja wa Ulaya amesema hiyo ni hatua muhimu kuelekea usafiri usiokuwa na vizuizi katika nchi wanachama hasa msimu wa jua.
Kama kusherehekea tangazo hilo wasimamizi wa mnara wa Eiffel mjini Paris wametangaza watafungua kitovu hicho cha kitalii Julai 16 baada ya miezi kadhaa ya kufungwa kwa sababu ya janga la COVID-19.

No comments:
Post a Comment