Search This Blog

Saturday, May 22, 2021

Pacquiao kupanda ulingoni kwa mara nyingine


Mwanamasumbwi, Manny Pacquiao anatarajiwa kupanda ulingoni kwa mara ya kwanza baada ya miaka miwili atakapokuwa akipigana na bingwa wa WBC na IBF uzito wa kati Error Spence mwezi August mwaka huu.

Pacquiao mwenye umri wa miaka 42, hajapigana pambano lolote tangu amchakaze Keith Therman alipokuwa akiwania ubingwa wa WBA uzito wa kati mnamo mwezi Julai mwaka 2019.

Kupitia akaunti yake ya Twitta , Pacquiao ambaye ni gavana wa jimbo nchini Ufilipino amethibitisha atapanda ulingo dhidi ya Spence mwenye umri wa miaka 31 .

Pambano hilo litakuwa ni la 72 kwa Pacquiao ambapo ameshinda 62, kapoteza 7 na sare 2 katika rekodi zake na anawania ubingwa wa Dunia katika mungo wa nne tangu atwae wa kwanza mwaka 1998 .

Spence ana rekodi ya kuvutia kwani ameshinda mapambano 27 na hajapoteza hata moja na pigano lake la mwisho lilikuwa ni dhidi ya Danny Garcia ambalo lilifanyika Disemba 2019.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...