Search This Blog

Saturday, May 22, 2021

Jela miaka 30 kwa kubaka Mwanae wa kufikia


Mkazi wa Kijiji cha Buchanchari wilayani Serengeti, Chegera Mayemba amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka mtoto wake wa kufikia.

Mayemba (35) amepewa hukumu hiyo na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Serengeti, Judith Semkiwa baada ya kujiridhisha na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo.

Mbali na ushahidi huo, pia mshtakiwa alikiri kutenda kosa hilo ambapo, Hakimu Semkiwa amesema kosa hilo adhabu yake ni miaka 30 jela huku akiacha wazi milango ya rufani.

Awali, Wakili wa Serikali na ambaye ni Mkuu wa Mashitaka Wilaya ya Serengeti, Mafuru Moses ameiambia mahakama kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Mei 12, mwaka huu.

Amesema baada ya kupitia jalada na kubaini ushahidi wa tukio hilo uko wazi kuwa Mei 21, mwaka huu, wamemfikisha mahakamani na baada ya kusomewa na kukiri akaomba mahakama kutoa adhabu kali kwa kuwa kitendo alichofanya ni cha kinyama.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...