Mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya ICC, Fatou Bensouda ameitaka serikali ya mpito ya Libya kumkatama mtoto wa kiongozi wa zamani wa Libya, Moammar Gaddafi, Seif al-Islam na kuwataka wapiganaji mamluki na wa kigeni kuondoka mara moja, tofauti na hivyo watakabiliana na mkono wa sheria kutokana na vitendo vya kihalifu.
Katika taarifa yake ya mwisho kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Libya Bensouda amesema ICC imeendelea kupokea taarifa za vitendo vya kihalifu vinavyoendelea nchini Libya, kuanzia kutoweshwa kwa watu, mauaji holela, watu kuwekwa vizuizini, utesaji pamoja unyanyasaji wa kijinsia.
Aidha amegusia tuhuma za matendo ya uhalifu ambayo yamefanywa na maafisa wa nchi hiyo katika maeneo ya vizuizi vya watu yasio rasmi, sambamba na kufanyika kwa hukumu za siri.
Libya imeingia katika machafuko 2011, baada ya majeshi ya umoja wa kujihami wa NATO kuunga mkono vuguvugu lililomuondoa madarakani Gaddafi na kuacha taifa hilo katika mgawanyiko hadi sasa.

No comments:
Post a Comment